Ijumaa , 20th Jan , 2017

Mwanamuziki wa Afro Pop toka Scotland Uingereza Iain Stewart ameuanza mwaka mpya 2017 kwa kuachia video ya wimbo wake uitwao 'Love again' akimshirikisha msanii toka Afrika Mashariki wa nchini Rwanda Mani Martin

Wimbo huu wa 'love again' ni wimbo unaoelezea mwanamke ambaye amewahi kuumizwa sana kimapenzi na anataka kumsaidia ili aweze kupenda tena.

"love again' ni wimbo wangu wa pili katika albamu yangu inayokuja, wimbo wangu wa kwanza kuuchia kwenye hii albamu unaitwa 'Nicheze Nawe'. Wimbo huu wa 'love again' umeimbwa katika lugha tatu ambazo ni Kingereza, Kinyarwanda na Kiswahili ili watu wote wanaosikia lugha hizi waweze kufurahia wimbo huu". Ameelezea Iain Stewart

Video ya 'love again' shooting yake imefanyika katika eneo la Galaxy Hotel na Inema Arts Center, Kigali, Rwanda.

Itazame hapa  https://www.youtube.com/watch?v=QPNjtgNkfRg