Alhamisi , 19th Jan , 2017

Muigizaji wa filamu za bongo Ray Kigosi amebahatika kupata mtoto baada ya mchumba wake Chuchu Hans kujifungua mtoto wa kiume.

Ray Kigosi akiwa na mchumba wake Chuchu Hans kabla ya kupata mtoto.

 

Ray Kigosi ambaye ameonesha kuwa na furaha kubwa kupata mtoto wa kiume amefunguka na kuwataka watu waache maneno yao kuwa mtoto amekunywa maji mengi kutokana na weupe wake na kusema kuwa mtoto huyo anaonekana hivyo kwa kuwa bado ni mdogo na kwamba ile ilikuwa ni kauli ya utani.

Kauli hiyo inaonyesha ni jinsi gani Ray Kigosi amefurahi kupata mtoto wa kiume ambaye yeye anamwita pacha wake.

Muonekano wa baadhi ya sehemu za mwili wa mtoto wa Ray

"Asante Mungu kwa kuniletea pacha wangu asante 'my lovely' Mzungu kwa kunipa heshima kubwa kunifanya niitwe baba, Mungu wangu wa haki asiyeshindwa na jambo akubariki sana. Sasa msianze maneno yenu kwamba mwanangu amekunywa maji, mtoto bado ni mchanga maana watu wa Insta kiboko lakini hawaishi mtoni". Aliandika Ray Kigosi