Alhamisi , 27th Aug , 2015

Baada ya kufunguliwa kwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Kamati ya Maandalizi ya Michuano hiyo imekuja na mikakati ya kurejesha hadhi na heshima ya mashindano hayo makubwa ya kusaka walimbwende nchini.

Katika kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa.

Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jokate Mwegelo ametoa shukrani kwa niaba ya kamati yake kwa kuamininiwa kupewa jukumu hilo na kuahidi maboresho makubwa na mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya Miss Tanzania.

Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao

1.Juma Pinto – Mwenyekiti

2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti

3.Doris Mollel – Katibu Mkuu

4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati

5.Hoyce Temu – Mjumbe

6.Mohamed Bawazir – Mjumbe

7.Gladyz Shao – Mjumbe

8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe

9.Shah Ramadhani – Mjumbe

10.Hamm Hashim – Mjumbe

11Khalfani Saleh – Mjumbe

12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni

1.Dr.Ramesh Shah

2.Hidan Ricco

3.Yasson Mashaka

4.Deo Kapteni