Alhamisi , 19th Jan , 2017

Rapa Roma Mkatoliki aliyejizolea umaarufu na kufahamika kwa kuimba ngoma zenye mlengo wa siasa na zenye kuleta changamoto kwa viongozi mbalimbali wa taifa amefunguka na kusema kuwa yeye hawezi kuacha muziki wa harakati.

Roma Mkatoliki

Amesema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa muziki huo ndiyo umempa heshima na mafanikio makubwa pamoja na imani kubwa kwa wananchi.

Roma Mkatoliki anasema hivi sasa ameamua kubadilika kidogo katika ngoma zake akiwa na lengo la kwenda sawa na muziki wa sasa lakini pia kutaka kuonesha kuwa anaweza kufanya jambo lolote kwenye muziki.

"Huo muziki wa harakati mimi ndiyo umenipa mafanikio na siwezi kuacha hata siku moja, kuna watu wengi wanafanya muziki huo mgumu lakini hawapati nafasi lakini mimi kila show kubwa nitakuwepo na kuimba ngoma hizo hizo na kusepa na kijiji changu, kwa hiyo ni muziki ambao unanilipa na umenipa mafanikio saizi najaribu kuonesha kitu tofauti ambayo siyo dhambi mwingine anaweza kuja na misimamo yake akasema mimi nimesimama hapa" alisema Roma Mkatoliki