Jumatatu , 18th Oct , 2021

Kutoka familia ya Kardashian, Kourteny Kardashian amevalishwa pete ya uchumba na Rapper Travis Barker usiku wa kuamkia leo.

Picha ya Kourteny Kardashian na Travis Barker

Baada ya kudumu katika mahusiano kwa miezi 10, Travis amemvalisha pete ya uchumba Kourtney katika fukwe za hotel ya Montecito nchini Marekani. Hii ni mara ya kwanza kwa Kourtney mwenye umri wa miaka 42 na watoto watatu, na mara ya 3 kwa Travis kumvalisha mwanamke pete ya uchumba.