Lulu Diva : Napenda kudekezwa

Saturday , 15th Jul , 2017

Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya Utamu, Lulu Diva amedai katika vigezo ambavyo anavyoangalia wakati wa kuingia kwenye mahusiano ni pamoja na mwanaume mwenye shahuku ya mafanikio lakini pia atakayeweza kumvulia na kuwa msikivu.

Diva huyo anayekuja kwa kasi kwenye 'game' ya bongo ameeleza kuwa licha ya kuhitaji mwanaume mwenye vigezo hivyo, lakini pia anapaswa kujua kwamba Lulu Diva ni msichana mrembo na anayependa sana kudekezwa.

“Mpaka mtu awe na mimi kwenye mahusiano kuna vigezo naviangalia. Kwanza kabisa nampenda mwanaume smart mind, mtu ambaye ameshika dini anamuheshimu Mungu, pia gentlemen kama hivyo awe ananidekeza awe ananijali, , understanding, passion na Sacrifice,"

Msanii huyo ambaye ni zao la warembo waliokuwa wakipamba nyimbo za wasanii kabla ya kugeukia tasnia ya uimbaji amesema pamoja na kupenda kwake kudekezwa haimaanishi kwamba anababaishwa na vitu vidogo vidogo, La! hasha yeye ni mrembo lakini pia mtafutaji anayejituma.

 

 

 

Recent Posts