Alhamisi , 30th Oct , 2014

Msanii wa muziki M2THEP, ameweka wazi kuwa kwa sasa moyo wake umefunguka na Stress zimekwisha kabisa tayari kwa kufanya muziki kwa nguvu zaidi, baada ya kutembelea kaburi la Marehemu Ngweair na kuzungumza na marehemu kwa imani juu ya yote waliyopitia

M2THEP

M2THEP amesema kuwa, kwa kuanzia hili, ameachia rasmi video mpya ya ngoma yake inayokwenda kwa jina Siyabonga Nkosi, ikiwa ni kazi kubwa kabisa na ya kwanza akiwa anaamini kuwa moyo wake una amani na hana stress tena zinazotokana na kifo cha Ngweair.

Katika mahojiano ya rapa huyu na eNewz, hivi ndivyo alivyofunguka kuhusiana na hili na video mpya ambayo unaweza kuitazama wakati wowote kuanzia sasa kupitia EATV.