Madee 'amfungia' binti yake Instagram

Friday , 21st Apr , 2017

Rais wa Manzese, Madee Seneida ameapa kutomuhusisha binti yake na mitandao ya kijamii kwa sasa bali anapambana kufanya kazi katika kuhakikisha anamtengenezea binti yake maisha na kumuwekea akiba ya pesa benk na siyo picha.

Madee

Akiwa EATV Madee amesema kuwa maisha yake binafsi hayahusiani na mitandao ya kijamii na ndiyo sababu ya kugoma kumfungulia mtoto wake akaunti ya instagram kama wasanii wengi wakubwa ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla.

"Mimi nilijua naulizwa kwa nini sijamfungilia mtoto wangu akaunti ya benk, kumbe tu ni akaunti ya Instagram jamani.... mimi  nitamfungulia akaunti ya benki na tayari nilikwishafanya toka alipozaliwa na siyo insta, mtoto mwenyewe nakaa naye mtaani siku 15 kati ya miezi sita hizo picha nitakuwa nampiga saa ngapi, hata mastaa wanaowafungulia watoto wao inaelekea wana muda wa kutosha lakini mimi muda sina na sitaweza kusimamia hata hiyo akaunti ya instagram yake na yangu ila akikua atafanya mwenyewe" - Madee.

Katika hatua nyingine Madee amekanusha vikali tetesi za kuwa na mtoto mwingine.

"Sina mtoto mchanga, bali nina mtoto mmoja ambaye ni Sada pekee na sula kama la kuwa na mtoto siwezi kulificha kwa sababu atakua... Mbona Sada niliwaambia. Kusema nina mtoto mwingine saizi ni mapema sana ingawa nina watoto wawili ambao ni Sada na Abdul-Aziz au Dogo Janja" Madee alimaliza.

Recent Posts

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan

Current Affairs
Kero za muungano kutatuliwa - Samia Hassan

Mtayarishaji na msanii wa muziki Quick Rocka 'Switcher'

Entertainment
Hakuna muziki mpya sasa - Quick Rocka

Nahodha msaidizi wa Azam FC, Himid Mao (Kulia) akiwa na mshambuliaji Mghana, Enock Atta Agyei (Kushoto)

Sport
Tupo fiti kuwavaa Simba Jumamosi - Himid Mao

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Current Affairs
Watanzania tudumishe Muungano - Balozi Seif Iddi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu

Current Affairs
Kupima Malaria sasa ni bure - Waziri Ummy Mwalimu