Alhamisi , 19th Jan , 2017

Msanii wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa kupitia  mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana hawaujui ukweli na wakiujua watatulia.

Madee

 

Akionge kupitia eNewz Madee amesema hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na ndipo hayo yakatokea.

"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee

 Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti. 

Hata hivyo Madee amesema uongo huwa hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu  wale ambao wamemtukana kwa kuwa hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu wote wataujua ukweli.