Jumatatu , 19th Jun , 2017

Msanii kutoka 'Tip Top Connection' Madee Ali amefunguka kwa kusema muziki wa kizazi kipya (bongo fleva) umepata kilema kutokana na kukosekana kwa tuzo pamoja na albamu za muziki.

Msanii Madee Ali

Madee amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya majigambo ya wasanii wengi wanaodai kutaka kuutangaza kimataifa zaidi kazi za muziki zinazofanywa ndani ya Tanzania.

"Muziki wetu umepata kilema, hauna tuzo hauna albamu halafu kuna watu wanasema wanataka kuufikisha mbele......Kwa njia gani labda" aliandika Madee.