Ijumaa , 19th Mei , 2017

Mtayarishaji wa Mkongwe wa Muziki Bongo, P. Funky Majani amemtaka Rapa Mkongwe Afande Sele kumuandikia mashahiri msanii Hamorapa anayechipukia kenye game ili kutimiza ndoto zake na siyo kumkatisha tamaa.

Majani amelazimika kumuomba Afande kufanya kazi hiyo baada ya kumdiss Harmorapa na kusema ''Harmorapa siyo msanii na hataweza kudumu kwenye 'game' ya bongo Fleva kwa muda mrefu".

Majani amefunguka hayo leo kwenye heshima ya bongo fleva ndani  Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa kwa kuwa tayari Afande anakofia ya ufalme wa mashahiri anapaswa kuwasaidia wadogo zake wenye shauku ya kusikika na siyo kuwakatisha tamaa huku akijiona yeye ndiye anafaa kuimba kuliko wengine.

"Afande namuomba kitu , kama unaona dogo anayumba hutakiwi kumbeza bali unapaswa kumuandikia mashahiri na kukuza sanaa yake. Wewe ni Mfalme wa Rymes unapaswa kuwasaidia wadogo zako ambao wanaonyesha juhudi zao binafsi za kujituma. Siyo lazima Afande ufoke wewe usikike wasaidie hawa wachanga wainuke wawe bora kama wewe usiwakatishe tamaa ukiwa wewe ni kaka yao"- P Funk alifunguka.

Aidha Majani ameongeza kwamba Harmorapa amebadilika kimuziki tofauti na alivyoanza hivyo ni vyema akazidi kupatiwa misaada mbalimbali ya kumkuza kipaji chake, huku akimwelezea ni kijana anayejituma, mwenye adabu, pia mwenye shauku ya kufika mbali kimuziki.