Jumatatu , 21st Aug , 2017

Msanii wa mwenye 'hit song' ya 'anameremeta', Nuh Mziwanda ameanza kupoteza muelekeo wa maisha yake kiujumla kutoka na kutendwa kipenzi mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada katika mitandao ya kijamii kwa kutaka achaguliwe mwanamke wa wa kumuoa tena.

Msanii Nuh Mziwanda.

Nuh aliweka wazi hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika "nimejifunza mengi sana kwenye 'life style' yangu ya kimapenzi na najitoaga sana, ila siku ya mwisho naumizwa 'je unahisi mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu naye? leo nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili". Jambo hilo baadhi ya mashabiki zake walilichukulia tofauti na kupelekea kutoa maneno yenye ukakasi kwa kile wanachokidai kutoridhishwa na mwenendo wa msanii huyo kutotaka kutuliza akili yake baada ya kupata maumivu ya kimapenzi mfululizo kutoka kwa watu ambao alikuwa akijihusisha nao kimapenzi.

Huu ndiyo ujumbe aliyoweka Nuh Mziwanda katika ukurasa wake wa Instagram.

Kutokana na hicho mashabiki zake walimshauri kwa kumtaka msanii huyo kuacha pupa ya kukimbilia kwenye mahusiano mapya na badala yake atulize akili yake katika kujipanga kimaisha pamoja na kutumia muda huo kumuomba Mungu ili aweze kumchagulia mke mwema nasiyo kama yeye alivyokuwa amefanya.

Maoni ya mashabiki zake.

Nuh Mziwanda katika siku za hivi karibuni ameonekana kuandamwa na jinamizi la kukataliwa kimapenzi na wasichana wawili tofauti ambao aliweza kuwaweka wazi ambaye ni Shilole pamoja na aliyekuwa mke wake wa ndoa Nawal ambapo inasemakana, Nuh Mziwanda alipigwa kibuti kutokana na kutokuwa na pesa za kutosha za kuweza kuihudumia familia ya mwanamke.