Jumatano , 11th Jan , 2017

Msanii wa bongo fleva Matonya amesema kwa sasa ugomvi uliokuwepo kati yake na muandaaji wa muziki Adam Juma umemalizika na kwamba akipata nafasi atafanya naye kazi tena.

Matonya

Tonya amesema "tulisumbuana sana na Adam Juma hali iliyopelekea kufikishana hadi polisi lakini kwa sasa tumeshakuwa kama familia"

Adam amefanya mabadiliko makubwa katika sanaa ya bongo fleva na sasa ameamua kufanya na waadaaji wengine ili aweze kubadilika.

Hata hivyo Matonya amesema anakubali muonekano wake kwa sasa na huwa havungi inapofikia kwenye swala la msosi ndiyo maana kila siku anazidi kunenepa na kitambi  kukua zaidi.