Jumatatu , 29th Mei , 2017

Meneja wa wasanii wa muziki wa Bongo maarufu kwa jina la Meneja Maneno ambaye amefunguka jinsi alivyomtoa msanii Sam wa Ukweli, na kuweka wazi kuwa alimkuta akiwa anauza matunda lakini aligundua kuwa ana kipaji na kuamua kufanya naye kazi 

Meneja Maneno alisema hayo kupitia kipindi cha 'Bongo fleva Top 20' cha East Africa Radio wakati akielezea aina ya mameneja wa wasanii waliopo nchini huku akisema wapo mameneja ambao wanawalipa wasanii na wapo mameneja wengine hawana uwezo wa kumlipa msanii bali msanii anawalipa hao mameneja.

"Niliajiriwa kwenye kampuni ya kusambaza albam za wasanii Tanzania katika harakati zangu za kusambaza kanda nilikutana na Sam wa Ukweli akiwa anauza matunda lakini alikuwa na kipaji ndiyo nikaja nikaachia ile ngoma 'Sina raha', tukaja tukaachia 'Hata kwetu wapo' akapata marafiki wapya tena watu waliomrubuni ni wale wale niliokuwa nao Aljazira wakamchukua kijana mwisho wa siku kipaji chake kikaenda kufa, wakamuweka kapuni unajua hata ukiwa na hela vipi kama njia huzijui msanii kudumu ni ngumu" alisisitiza Meneja Maneno 

Mbali na Sam wa Ukweli, Meneja Maneno pia amewahi kuwasimamia wasanii kama ama Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Diamond Platnumz

Meneja Maneno