Jumanne , 21st Feb , 2017

Meneja wa kundi la Yamoto band Mkubwa Fella amekiri kuwa ajira katika taifa letu ni gumu ndiyo maana yeye ameamua kujenga kituo ili kuwasaidia vijana kuondokana na makundi mabaya na kuweza kujiajiri kupitia muziki. 

 

Mkubwa Fella anasema amekutana na baadhi ya viongozi wa serikali kama Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nauye na kumshauri kujenga kituo kama chake ili kuweza kuwasaidia vijana waweze kujiajiri kupitia muziki.

Msikilize hapa Mkubwa Fella alipokuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV na EA Radio kikitangazwa na Dullah Planet , alipokuwa akitambulisha rasmi kundi jipya la muziki, linalokwenda kwa jina la 'Madada Sita'