Jumatano , 18th Jan , 2017

Msanii wa bongo fleva Mo Music amewasihi wasanii wezake kutengeneza nyimbo nzuri badala ya kutafuta kiki mbalimbali ili kutengeneza 'hit song' huku wakitengeneza nyimbo mbaya zisizo na ujumbe wowote kwenye jamii.

Mo Music

Akiongea kupitia eNewz Mo Music mwaka 2016 haukuwa mzuri sana kwenye maisha yake kwa kuwa alikuwa na kesi mahakamani na aliyekuwa mchumba wake.

Hata hivyo Mo Music hakusita kuwashukuru mashabiki zake  wanaomsapoti kwa mwaka 2016  na kuwaahidi kuachia nyimbo kali na kuwapatia mashabiki zake kile wanachokipenda kutoka kwake