Ijumaa , 15th Oct , 2021

Aryan Khan (23) mtoto wa nyota wa filamu za Bollywood Shah Rukh Khan, ataendelea kusota jela baada ya kukosa dhamana kutoka Mahama maalum ya mjini Mumbai nchini India kutokana na msala wake wa dawa za kulevya unaomkabili.

Picha ya Aryan Khan mtoto wa nyota wa filamu za Bollywood Shah Rukh Khan akiwa na Maafisa wa NCB

Mtoto huyo alikamatwa kwa kuhusishwa kwenye tukio ambalo dawa za kulevya zilipatikana kwenye meli iliyokuwa ikielekea pwani ya Mombai ambapo taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya NCB inadai kuwa Aryan alikuwa mtumiaji wa kawaida wa dawa zilizozuiliwa na Taifa hilo kwa miaka kadhaa.

Sasa Aryan atalazimika kukaa jela mpaka Oktoba 20 kutokana na Mahakama Kuu na Vikao vya Mahakama kufungwa kuanzia Oktoba 15 - 19 kwa sababu ya sikukuu ya Dussehra.