Ijumaa , 10th Oct , 2014

Mwigizaji maarufu kutoka Uganda, Abby Mukiibi ambaye nyota yake iling'ara sana kupitia ushiriki wake katika filamu ya The Last king Of Scotland, amepata shavu jingine kubwa la kushiriki katika filamu ya kimataifa.

muigizaji nyota wa Uganda Abby Mukiibi

Katika maelezo ya awali, imefahamika kuwa Abby atashirikiana na Timu kutoka Uholanzi pamoja na Watayarishaji mahiri wa filamu huko Senegal kwa ajili ya kuifanya kazi hiyo.

Filamu hiyo inatarajiwa kubeba kisa kingine cha aina yake kuhusiana na Bara la Afrika.