Jumanne , 28th Mar , 2017

Mwanamuziki wa kimataifa wa nyimbo za injili, Timotheo Mulonda Denis ‘TMD’ amefungukia sababu ya kutumia kipaji chake kwenye nyimbo za injili ni kutoa shukrani kwa Mungu aliyemuumba pia kuwakumbusha watu wa rika zote kuacha dhambi na kumkumbuka Mungu

Timotheo Mulonda Denis ‘TMD’

Timotheo ambaye ni mtanzania ila kwasasa makazi yake makuu yapo 'Dublin Ireland’ amesema alianza kutumika kumuimbia Mungu tangu alipokuwa mtoto na hata kabla ya kujiunga na kwaya ya kanisa alikuwa akitengeneza ala za muziki kwa kutumia makopo yeye pamoja na watoto wenzake wakati wa michezo.

“Nampenda yesu, nilianza kazi ya uimbaji nikiwa mtoto sana, Tulikuwa na watoto wenzangu tukipiga vikopo kama instrument, nilijiuga na kwaya ya watoto kanisani ambako walinisajili kwenda kuimba na Band kubwa ya kanisi ambapoo nilihudumu kama ‘Vocal leader’ wa Band hyio kwa miaka mingi sana, Ilifika kipindi nikajiunga na kwaya kubwa ya kabisa huko nilianza uwandishi wa nyimbo na uongozi pia. Muziki wa Gospel upo ndani ya damu” – Mulonda.

Msanii huyo ambaye kampuni yake inaandaa na kuinua vipaji vya waimbaji wa injili nchini Ireland  amewahi kuimba nyimbo nyingi kwa lugha mbalimbali  ikiwemo  kiswahili,kifaransa, kingereza, kilingala, Kimbembe, na lugha zingine kutoka Afrika.

“ Mimi naimba kwa kutumia lugha nyingi  tofauti tofauti lakini Kiswahili ndio Lugha inayo beba muziki wangu  kama kwenye Mirror, Lumamba, Baba nimekosa, give a place, is gonna be alright, na nyingine nyingi zilizokuwa katika Album yangu ya kwanza zimebebwa na kiswahili”. Lumonda aliongeza.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha ‘Amejibu’ kilichoandaliwa na Producer Terrence Mugwande / Rejoice studio ya Terrozone  amedai kwa sasa anaendelea kuandaa albam yake ya pili itakayokwenda kwa jina la Chozi lako ‘ Your Tears’.

Waweza tazama hapa wimbo wake wa amejibu https://www.youtube.com/watch?v=FUNY-xbuqck