Ijumaa , 20th Jan , 2017

Rapa Suma G ambaye aliwahi kutamba na ngoma kibao kali kama 'Vituko uswahilini', Demu wako na pia alikuwa akiunda kundi la Hotpot Family amefunguka na kusema mpaka sasa anaendesha maisha yake kwa muziki.

Suma G

 

Suma G akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio amesema mpaka leo anapata show na kufanya show mikoani na kupata pesa ambazo zinamsaidia kuendesha maisha yake ya kila siku.

"Nipo kwenye muziki ingawa mara ya mwisho kutoa kazi mpya ni kama miaka miwili hivi, ila mpaka sasa naendelea kufanya movements za muziki na muziki huohuo unafanya niendelee kuishi mpaka leo. Huwezi amini mimi naendelea kufanya show sababu muziki tuliofanya kipindi hicho ulikuwa mkubwa ndiyo maana mpaka leo naweza kufanya show na kupata riziki yangu" alisema Suma G. 

Mbali na hilo Suma G anasema licha ya kutotoa kazi mpya muda mrefu lakini mashabiki wamekuwa wakimpokea vyema kila anapokwenda kufanya show mikoani.

"Muda mwingi nafanya show ambazo naziandaa mimi mwenyewe, huwezi amini muziki wangu unaendelea kufanya vyema kila kona nayokwenda, kwa hiyo sijashiriki matamasha makubwa mengi nimekuwa na timu yangu tunajipanga tunakwenda tunashambulia tunapata riziki yetu tunarudi mjini na maisha yanaendelea" alimazia Suma G