Mchekeshaji Mkojani
Mkojani amesema ndoa yake ilipangwa kufanyika mwezi wa 3 mwaka huu lakini kutokana na mipango na sababu za kifamilia ikashindikana kufanyika, na lengo la kufanya harusi yake kwenye meli ni kutaka iwe na ukubwa wa aina yake.
"Nina mipango ya kuoa, ndoa yangu ilikuwa ifanyike mwezi wa 3 lakini sababu za kifamilia ikashindikana, harusi yangu nataka niifanye kwa ukubwa fulani iwe ndani ya meli na ya kitajiri, nadhani mwezi wa 6 au 7 itakuwa tumeshakamilisha hilo jambo, mchumba wangu tayari naishi nae na nimeshatoa barua" amesema Mkojani
Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.