Jumatano , 29th Mar , 2017

Msanii Roma Mkatoliki amesema hali ya utandawazi imeharibu nchi ya Tanzania katika utendaji kazi maofisini mpaka shuleni kutokana na watu kutekwa na mitandao  ya kijamii kwa kutotaka kupitwa na vitu vinavyoendelea kutokea.

Roma

Akizungumza katika kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV rapa huyo anayetamba na ngom ya 'Usimsahau Mchizi' ametoa kauli hiyo kufuati hali ya nchi kukumbwa na matukio makubwa ya kisiasa kila kukicha na kupelekea kila mwananchi kutamani kuona au kusikia mwenyewe.

“Hali ilipofikia sasa hivi ni heri mtu akose figo kuliko bando nikimaanisha kwamba nguvu ya mitandao kijamii  imekuwa kubwa sana kiasi kwamba ukienda mashuleni, maofisini utakuta watu saa 12 asubuhi wakiripoti maeneo yao, mchongo wa kwanza utakuta mtu anakwambia ebwana umeona fulani instagramu ameandika nini, kitu kama hicho kuanzia mwaka 2012 kushuka chini sijawahi kukiona”. Alisema Roma

Aidha msanii huyo amejitolea mfano kwa kusema imefikia hatua endapo wanapokutana na washkaji zake basi ndani ya dakika 40 wote wanajikuta wamepiga ukimya (ganzi) kila mtu huwa yupo ‘busy’ na simu yake kuangalia ‘ubuyu’ katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande mwingine Roma amefafanua ile kauli yake aliitoa kuwa ‘tunajenga Tanzania ya viwanda au Tanzania ya ubuyu’ na kusema laiti kama watanzania wote wangekuwa wapo pamoja katika kutazama huko basi lengo hilo la kubadirisha nchi ingekuwa nyepesi lakini sasa hivi imekuwa tatizo kubwa kutokana watanzania wengi kuwa hawajapewa nafasi ya kutoa mawazo yao katika kuiboresha na kuijenga dhana hiyo katika nafasi inayostahili.