Jumanne , 5th Jul , 2022

Hitmaker wa ngoma ya masebene Y Tony amefunguka kilichotokea baada ya kuingia kwenye jeneza wakati anafanya show jukwaani.

Picha ya msanii Y Tony

Akizungumza na PlanetBongo ya East Africa Radio Y Tony amesema
 
"Mnapokutana kwenye show wasanii wengi lazima uweke ubunifu tofauti, ilikuwa emotion ngumu sana nilikuwa naweweseka wiki mbili kulala ndani ya jeneza na kufunikwa ni kitu kizito nashukuru Mungu ile hali ilipotea".

"Ubunifu wa kupanda na jeneza nilifanya mwenyewe, niliingia ndani ya jeneza kwa dakika 2 jukwaani lakini cha ajabu ndani ya jeneza kulikuwa na baridi, sikufanya kama kiki nilifanya kitu kilichopo kwenye kazi yangu".