Jumatatu , 21st Aug , 2017

Muongozaji wa video nchini, Nisher amesema bado anashangazwa na watu wanaodai yeye alikuja kuchukua (crown) ya Mkongwe Adam Juma katika uongozaji wa video za muziki kwani hakuna anayeweza kufanya hivyo na kushauri watu wasome historia.

Director Nisher

Nisher amesema hayo kupitia mitandao ya kijamii alipoamua kujibu maswali ya mashabiki zake ambayo yamekuwa yakiulizwa ambapo Nisher amesema  hata sasa hivi Adam Juma anaweza kufanya video kali kwani hakuna aliyechukua crown yake na zaidi ni kwamba tayari Adam alishatengeneza 'brand' yake.

“Mpaka leo kuna ambao wanasema mimi nilimfukuza Adam Juma kwenye music video industry, siwezi kumfukuza Adam Juma, nimekuta ana C.V yake ndefu inatisha, namuheshimu siku zote siwezi nikakaa niseme nimekuja kuichukua crown ya Adam Juma na the game is big enough for the both side, industry ni kubwa kiasi kwamba inatutosha watu wote kila mtu anaweza kuwa na crown," Nisher.

Nisher akiwa na Mkongwe Adam Juma

“Mimi na uwezo wa kunyamaza mwaka mmoja au miezi kadhaa nisitoe video lakini nikitoa video imetua, ni kwa sababu nimeshajenga hilo jina kwa takribani miaka saba sasa hivi, nobody can take my crown, nobody can take Adam Juma's crown,” amesema Nisher.

Pamoja na hayo Nisher ameongeza kuwa anaamini muda na wakati wowote Adam Juma akitaka kurudi kwenye game anaweza japo kuna changamoto za biashara ambazo yeye anaamini haina kufeli.

“Adam Juma sasa hivi akiamua kupiga video inatoka kali, amerudi, so hakuna kukosea, hakuna kufeli. Biashara tu inakupanda na kushuka, kuna wakati ni high season na kuna wakati ni low season, its business,” amesisitiza.

Pamoja na hayo Nisher amewataka mashabiki wasome pamoja na kufuatilia historia mbalimbali ili wasiweze kuchanganya mambo ambayo hayawezi kufutika katika historia