Jumapili , 21st Mei , 2017

Msanii wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aka baba Anyagile anayetamba na ngoma yake ya 'Anameremeta', anatamani mwanae akiwa mkubwa asiwe maarufu bali awe mtu wa kawaida tu na wala asizuzuke na ustaa wa baba yake.

Nuh amekaririwa hivi karibuni akisema kuwa hatamani mwanaye Anya arithi aina yoyote ya maisha yake ikiwa ni pamoja kurithi kazi yae bali atajitahidi kumpatia elimu ili aweze kuwa msomi.

“Mwanangu najitahidi kumtengenezea mazingira tangu mwanzo yale ambayo yeye baadaye yasije yakamkarahisha au akajiona yupo tofauti na watoto wenzie, hicho kitu cha kwanza that is why sipendi kumpublish sana kwenye mitandao ya kijamii. Pia nataka awe msomi , sitegemei mwanangu aje kufanya muziki wa Bongo Flava au mwanangu sitaki arithi chochote kutoka kwangu hata lifestyle yangu sitaki arithi”- alisema Nuh.

Pamoja na hayo Nuh amefunguka kwamba “Hata kuchora tattoo sitopenda mwanangu aje achore kwa sababu naamini sio kitu kizuri ingawa mimi mwenyewe nimechora na zina maana kwangu lakini sitopenda mwanangu aje afanye hvyo"- Nuh alifunguka zaidi