Alhamisi , 26th Nov , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Abubakar Kunenge ametembelea studio na ofisi za 'Konde Gang HQ' Mbezi Beach, chini ya msanii Harmonize ili kushuhudia utendaji wa kazi kisha kumshauri mambo kadhaa.

Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Kunenge, kushoto ni msanii Harmonize

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Kunenge, amemshauri msanii Harmonize mambo mbalimbali ikiwemo kujituma, kuongeza ubunifu, ufanisi na nidhamu ya kazi.

Ikumbukwe kwa sasa Abubakar Kunenge ndiyo mlezi wa lebo ya Konge Gang chini ya boss wa lebo hiyo Harmonize akiwa na wasanii wengine watano.

Harmonize ameanzisha lebo hiyo mwaka huu baada ya kutoka kwenye uongozi wake wa mwanzo na mpaka sasa ameweza kusaini wasanii wengine ambao ni Ibraah Tz, Young Skales, Country Boy, Cheed na Killy.