Ijumaa , 21st Nov , 2014

Romy Jones, DJ Rasmi wa msanii Diamond Platnumz, ameweka wazi sababu za yeye kuacha kuimba kama alivyokuwa anafanya kipindi cha nyuma, na kusema kuwa hii ni kutokana na yeye kutokujisikia kuendelea kufanya hivyo.

msanii ambaye pia ni Dj wa Diamond Rommy Jones

Romy ambaye ameamua kukaa pembeni kumsapoti mdogo wake pia amezungumzia uzoefu wake katika kum-DJ msanii kama Diamond ambaye anashikilia rekodi ya kufanya maonyesho makubwa ndani na nnje ya nchi, kazi ambayo amesema inahitaji kuwekeza akili zote katika kuwapa watu burudani ya kurudhisha.