Ijumaa , 20th Jan , 2017

Msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki ameseama katika historia ya maisha yake kimuziki hajawahi kubebwa wala kusaidiwa na msanii yeyote wa hapa nchini.

Roma Mkatoliki

 

Akiongea kupitia eNewz, Roma amesema katika maisha yake hakuwahi kusaidiwa hata 'kolabo' hivyo asije akasimama msanii yeyote akasema kwamba amemsaidia kimuziki japo hiyo haisababishi kumfanya yeye ashindwe kusaidia wasanii wengine wachanga.

Hata hivyo Roma amesema kwa sasa anampango wa kuanzisha kitu kitakachofahamika kama 'WWW' (watu wa watu) kwa kuwa anaamini yeye ni mtu wa watu hata asipotoa nyimbo kwa mwaka mzima lakini bado akiandaa show wananchi wanasimama na kumshangilia hivyo ataanzisha kwa ajili ya kuwasapoti wasanii wachanga japo bado haijawa rasmi