Jumapili , 21st Mei , 2017

Muimbaji na Muigizaji bongo, Snura Mushi amewataka wazazi kutowabana watoto wao kufanya sanaa kwa kuhofia ni uhuni na kudai tabia hizo ni hulka ya mtu na sanaa ni kazi kama zinginezo zinazowez kum,patia kipato kizuri na akaishi vizuri.

Snura amefunguka hayo kwenye Story tatu ya Planet Bongo na kusema kwamba uhuni ni tabia ya mtu mmoja mmoja na siyo sanaa nzima huku akidai kwamba wenye tabia hizo hata kama wasingekuwa wasanii uhuni wangeufanya kwenye biashara zingine zozote.

Snura ameendelea kutetea sanaa na kusema kwamba yeye binafsi amefanikiwa kuendesha maisha yake kwa kutumia sanaa huku akimlea mama yake pamoja na familia yake huku akitoa zaidi mifano ya kwamba wasanii wengi wamekuwa msaada kwenye familia zao kwa kupitia sanaa.

Katika hatua nyingine Snura amewaasa wasanii wachanga wanaotaka kujiingiza kwenye sanaa, waingie na kutafuta pesa na siyo kujiingiza kwenye makundi ya kihuni ambayo mengi yanasura ya kuchafua tasnia ya sanaa.

Msikilize Snura hapa chini akifunguka kutetea sanaa.