Jumanne , 16th Sep , 2014

Mkali wa miondoko ya R&B nchini Tanzania, Steve R&B ameweka wazi kuwa hivi sasa baada ya kukamilisha ratiba kadhaa za shughuli zake za kimuziki nje ya nchi, kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya harusi yake ambayo itafanyika mapema mwezi ujao.

msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Steve R&B

Steve R&B ambaye shughuli yake ya harusi imecheleweshwa na ziara zake nje ya nchi, pia amesema kuwa, sambamba na mipango ya harusi, tarehe 18 mwezi huu anatarajia kuwazawadia mashabiki wake ngoma mpya inayokwenda kwa jina Pole Pole.