Jumatano , 24th Feb , 2021

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini Tanzania Waziri Sonyo amefariki dunia siku ya jana Februari 24, baada ya kutoka kuangalia mechi ya ligi ya mabingwa Africa kati ya Simba na Al Ahly.

Picha ya aliyekuwa msanii wa muziki wa dansi Waziri Sonyo

Akitoa taarifa za msiba huo kupitia EATV & EA Radio Digital, mchambuzi wa muziki Rajab Zomboko ameeleza kuwa 

"Ni kweli amefariki jana, ametoka kuangalia mpira wa Simba alivyofika nyumbani kwake presha ikampanda na wakajaribu kumpepea lakini imeshindikana, msiba upo nyumbani kwake Kibaha Mailimoja, kuhusu mazishi nimeongea na ndugu zake wameniambia watanijulisha"

EATV & EA Radio Digital inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu pia wapenzi wa muziki wa Dansi hapa nchini.