Jumanne , 27th Sep , 2016

Msanii wa bongo fleva Tunda Man amewaomba radhi mashabiki zake baada ya kuwa na skendo ya kuzusha mambo yasiyo ya kweli.

Tunda Man

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kutangaza kuwa yuko location aki'shoot movie ya “Mama Kijacho”, kwa kudai kuwa yuko pamoja na Riyama Ally na Mboto huku wasanii hao wakikanusha kushiriki katika filamu hiyo.

Akipiga story na eNewz Tunda amesea 'Mimi nilikuwa nikijaribu kulinda idea yangu ya Mama Kijacho isiibiwe na watu wengine, kwa kuwa bado nilikuwa sijalisajili'.

Tunda amesema alizusha uvumi huo ili kuzuia wasanii wengine wasitamani kufanya movie inayofanana na idea yake, lakini pia alitamani kutengeneza movie hiyo ila alidai kuwa alishindwa kutokana na kukosa ushirikiano toka kwa wasanii wengine.

Alisema “Naona watu kama hawanipi ushirikiano, wanaona kama nitapata pesa sana, hivyo nimeamua kuachana nao”.

Lakini pia Tunda hakusita kuzungumzia ngoma yake mpya ambayo alikuwa akiitangaza mitandaoni muda mrefu uliopita inayojulikana kwa jina la Mwanaume suruali, alisema “Video nili'shoot Mombasa lakini yule mtoto ambaye nili'shoot naye alikuwa mke wa mtu na hakutakiwa kuonekana katika video yeyote, hivyo ikanichelewesha kuachia ngoma hiyo”.