Alhamisi , 25th Mei , 2017

Mfalme wa kisingeli Tanzania, Msaga Sumu amefunguka kwa kusema wimbo wake mpya wa ‘mwanaume mashine’ si fumbo lenye matusi kama baadhi ya watu wanavyodhani bali alimaanisha mwanaume mchapakazi na mtafutaji.

Msaga Sumu amefunguka kutatua utata wa neno hilo kupitia eNewz ya EATV baada ya watu wengi kuhukumu kuwa muziki wa singeli umejaa lugha chafu zenye matusi ambazo hazina maadili kwa jamii .

“Watu wengi inaonekana wanachukulia mwanaume mashine tofauti lakini jina la mwanaume mashine ni mwanaume mtafutaji, mchapakazi mfano angalia tu ile mashine ya kusaga inaweza kung’uruma kutwa nzima inakoboa mahindi tu.....Mimi sioni ajabu kuambiwa mwanaume mashine na ukiangalia mbona tunaimba mara moyo mashine mara sijui nini kwa hiyo mtu yoyote anayetafsiri vibaya ni bora aje aniulize mwenyewe mwanaume mashine inamaana gani". Alisema Msaga Sumu

Mtazame mwenyewe hapa anavyofunguka zaidi