Kushoto ni msanii Wakazi, kulia ni Gigy Money
Wakazi ameeleza kuwa Gigy Money ni mama wa mtoto pia anategemewa na familia yake, pia kuna wasanii wengine wanafanya mambo kinyume na maadili wanaachwa huru ila wanawaangushia jumba bovu wengine ambao hawana hatia.
"Kuna wasanii tena wakubwa wanafanya mambo ya ajabu, kinyume na maadili tuliyoyazoea, wanaachwa huru halafu Gigy Money ambaye alitumia ubunifu wa mavazi akashutumiwa yupo kinyume na maadili na kufungiwa miezi 6, Gigy Money ni mama anayetegemewa na mtoto na family yake it's not fair"
"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amefungulia vyombo vya habari, nadhani watendaji wake nao wawafungulie wasanii waliokatazwa kufanya sanaa kimakosa kama Gigy, halafu tukae vikao vya kufanya maboresho ya kanuni, sheria, sera na mengineyo ili sanaa iende na wakati, ikue kiubunifu na iwanufaishe wote wanaoifanya ili nao waweze kusaidia familia zao, na pia kulijenga Taifa" ameeleza msanii Wakazi