Jumanne , 28th Feb , 2017

Msanii wa kike ambaye pia ni 'muuza nyago' katika video za Kibongo, Lulu Abbas 'Lulu Diva' amefunguka na kutaja wasanii wake watano wa Bongo ambao anawakubali zaidi na kupenda kazi zao.

Lulu Diva amewataja wasanii hao alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema yeye anavutiwa zaidi na Vanessa Mdee, Belle 9, Dogo Janja, Madee pamoja Barnaba Classic. 

Mbali na hilo Lulu Diva amesema kwa kuwa ameingia kwenye muziki sasa hivi atafanya muziki mpaka siku pumzi zake zitakapokata na kusema mashabiki wakae mkao wa kula kwani atakuwa anashusha kazi kwa ajili yao.

Itazame hapa kazi mpya ya Lulu Diva