Jumamosi , 24th Jun , 2017

Msanii wa filamu nchini, Wastara Juma amepatwa na matatizo ya kiafya akiwa nchini Kenya alipokuwa ameenda kufanya kazi zake na kupelekea kulazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu.

Msanii Wastara

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo inadaiwa Wastara aliweza kupoteza fahamu kutokana na hali yake , ambayo huwa inamtokea mara kwa mara na maumivu ya mgongo.

Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa na uongozi wake kupitia ukurasa wa Instagram anaoumiliki yeye mwenyewe umesema mpaka sasa hali yake siyo nzuri hivyo kuwataka watanzania wamuombee ili aweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

                           Huu ndiyo ujumbe uliyoandikwa na uongozi wake.