Jumatano , 22nd Oct , 2014

Mwili wa msanii 'YP' ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam, umezikwa leo kwenye makaburi ya Chang'ombe.

msiba wa msanii YP wa kundi la TMK Wanaume Family uliofanyika Temeke Chan'gombe DSM

Mwili wa marehemu YP uliagwa leo mchana huko TCC Sigara Chang'ombe ambapo wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya burudani walihudhuria mazishi ya msanii huyo kutoka kundi la TMK Wanaume Family.

Mungu ailaze roho ya marehemu YP mahala pema Peponi. Amen.