Jumatatu , 16th Jan , 2017

Mwanamuziki Z-Anto ambaye aliwahi kufanya vyema katika muziki miaka ya nyuma na kuamua kukaa pembeni huku akifanya biashara zake ameanza vyema mwaka 2017 kwa kujenga nyumba ya nne nje ya kazi yake ya sanaa.

Z-Anto

 

Z-Anto ambaye makazi na shughuli zake za kila siku zipo Kigamboni Dar es Salaam, amefunguka na kusema ameamua kuanza mwaka 2017 kwa kujenga nyumba yake ya nne ambazo amejenga nje ya kazi yake ya muziki na sanaa kiujumla.

"Wiki mbili za mwanzo za mwaka 2017. House namba 4. Mwaka ndivyo tulivyouanza. #Thnxgod nje ya sanaa" aliandika Z Anto 

Z-Anto mwaka kupitia kipindi cha Planet Bongo aliahidi kurudi kwenye muziki na kusema kuwa label mbalimbali kubwa nchini zaidi ya nne zimemfuata ili wafanye kazi na kusema yeye anahitaji kuchanganua ili ajue ni label ipi ambayo inaweza kumpeleka mbali kimuziki na kufikia malengo yake kwenye muziki. 

Hizi ni baadhi ya nyumba zinazomilikiwa na Z-Anto