Jumanne , 2nd Apr , 2019

Wakati ikiwa imezoeleka kuwa nchi nyingi za afrika hufanya mila ya ukeketaji wa wanawake, hali imekuwa tofauti nchini Rwanda, kwani wao mila yao sehemu nyeti haikatwi badala yake hurefushwa hadi kufikia urefu wa kidole cha kati cha mkono.

Jinsi mila hii inavyofanyika

 

Mila hiyo inafahamika kama 'gukuna', ambayo hufanywa na shangazi au mama wa mtoto wa kike.

Mila hii ambayo inaonekana kuanza kutoweka kwa vijana wa sasa lakini inashamiri kwa wanawake ambao hawakuitekeleza wakiwa watoto, ikiwa na lengo hasa la kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa ili mwanamke aridhishwe zaidi.

Wanaume wa nchini Rwanda wamekaririwa wakisema kuwa ni muhimu kwa mwanamke kuridhishwa kwenye tendo la ndoa kuliko kuridhika wao pekee, na iwapo watashindwa kumridhisha basi hurudishiwa mahari yako au kunyang'anywa mke.