Alhamisi , 24th Apr , 2014

Mdhamini mkuu wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara Vodacom ametangaza kuipa klab ya Azam FC kitita cha shilingi milioni 75 baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Azam FC wakishangilia goli katika moja ya michezo yao ya ligi kuu ya Tanzania Bara ya msimu uliomalizika

Mdhamini mkuu wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara Vodacom ametangaza kuipa klab ya Azam FC kitita cha shilingi milioni 75 baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Akitangaza zawadi mbalimbali kwa mshindi wa pili Yanga anayepata shilingi milioni 37 wa tatu,timu ya Mbeya City anapata shalingi milioni 26 na ya nne Simba inapata shilingi milioni 21 Meneja Uhusiano wa Vodacom, Salum Mwalimu,ametaja pia zawadi kwa ajili ya wachezaji bora.

Amesema mchezaji bora atavuna Milion 5.2, mfungaji bora pia atapata Milion 5.2, mlinda mlango bora milion 5.2 pia na mwamuzi bora na Mwalimu bora watapata milion 7.8 kila mmoja.

Amesema kuwa Jumla ya zawadi zote kwa msimu huu ni Milion 210 kwa ajili ya timu zilizoshika nafasi nne za juu pamoja na timu nyingine zilizoonesha umahiri katika maeneo mengine ikiwemo timu yenye nidhamu itakayovuna Milion 16.

Mwaka jana bingwa wa Ligi Kuu (Yanga) ilizawadiwa kitita cha shilingi Milion 70.

Salum Mwalimu, amesema ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa ukilinganisha na msimu uliopita.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya ligi hiyo, Silas Mwakibinga, anasema licha ya changamoto nyingi katika ligi ya msimu huu ushindani ndio jambo la msingi katika maendeleo ya mpira nchini.

Sherehe za kukabidhi zawadi hizi, zitafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Mei