Jumatatu , 29th Mei , 2017

Mlinzi kilaka wa klabu ya Simba Abdi Banda amesema anaondoka klabuni hapo kwa kuwa makataba wake umeisha na hakuna mazungumzo yanayoendelea kati yake na uongozi wa wekundu hao, hadi sasa.

Abdi Banda wa kwanza (kushoto), akiwa na wachezaji wenzake wa Simba baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho

Banda, aliwashukuru mashabiki wa Simba na kuwaaga kwenye ukurasa wake wa Instagram, mara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao na kutwaa kombe la TFF Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Jumamosi iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Banda amesema viongozi wa Simba hawaoneshi kumuhitaji kwani hawajazungumza naye hadi sasa.

"Ni kweli naondoka kwa sababu mkataba wangu umeisha na hakuna kiongozi aliyezungumza na mimi kuhusu mkataba mpya, na ndo maana niliwaaga mashabiki wa Simba kwenye Instagram". Alisema mlinzi huyo wa zamani wa Coastal Union.

Kuhusu wapi anaelekea kwa maisha mapya ya soka, Banda alisema kuwa anataka kuelekea Afrika Kusini kucheza soka huko.