Jumanne , 19th Sep , 2017

Bayern Munich imethibitisha kuwa golikipa wake namba moja Manuel Neuer atakuwa nje ya uwanja hadi mwakani kutokana na kuumia mguu wa kulia.

Neuer ameumia jana kwenye mazoezi ya timu yake ikijiandaa na mchezo wa leo dhidi ya Schalke 04. Daktari wa Bayern Munich amethibitisha kumfanyia upasuaji wa awali mapema leo na ameumia eneo lile lile aliloumia mwishoni mwa msImu uliopita kwenye mchezo wa UEFA dhidi ya Real Madrid ambalo ni kifundo cha mguu wa kulia.

Mwenyekiti wa Bayern Munich  Karl-Heinz Rummenigge amesema Bayern itaathirika kwa kumkosa Neuer kwa takribani msimu mmoja lakini hawana namna lazima wazingate afya yake kwahiyo ni busara kumwacha apone kabisa.

Nohodha huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 31 amekuwa msaada mkubwa kwa klabu yake hususani kwenye michezo mikubwa.