Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Rais wa Philadelphia 76ers, Daryl Morey amesema kuwa mchezaji wao aliyegoma kucheza kwenye viunga vya Pennyslavania, raia wa Australia, Ben Simmons bado anahitajika kwenye kikosi chao licha ya mashabiki na baadhi ya wachezaji wenzake kuchoshwa na vibweka vyake.

(Nyota wa Philadelphia 76ers, Ben Simmons akiruka juu na kutupia mpira kwenye kikapu)

Kwa muda mrefu Morey ameelezea matakwa na matamanio kama kiongozi wa 76ers, kuwa ni kuunganisha timu kwa kumbakisha Simmons na watamuuza iwapo watapata timu iliyotayari kubadilishana nao kwa mchezaji mwenye uwezo unaowiana.

“Kwa sasa sote tunabidi tuungane, Kazi yangu kama Rais ni kuhakikisha naongoza jumuiya hii kushinda taji la NBA  msimu huu kwakuwa tunatimu nzuri, Simmons ni mchezaji anayeongeza kitu kikubwa kiwanjani kutokana na uwezo wake mkubwa”

“Iwapo tukiweza kumbakisha basi tutakuwa katika nafasi nzuri ya kunyakuwa ubingwa na iwapo itajitokeza timu kuhitaji huduma ya Simmons tutahakikisha kuwa ni kwa faida za pande zote mbili”

Simmons aliripoti katika kituo cha mazoezi cha timu hiyo siku ya  Alhamisi, Oktoba kwa mazoezi ya kibinafsi ambayo hakushiriki kwa sababu ya maumivu ya mgongoni  mwake. Simmons aliripotiwa kupata matibabu kutoka kwa wafanyikazi wa matibabu wa Sixers, ambayo pia ilimruhusu kuanza kufanya mazoezi.