Jumamosi , 14th Oct , 2017

Uhasama wa makocha Pep Guardiola wa Manchester United na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hospurs umeibuka tena baada ya wawili hao kujibizana kupitia mikutano ya waandishi wa habari hapo jana.

Mauricio Pochettino amemtuhumu Guardiola kuwa katika mkutano wake wa jana na waandishi wa habari aliikejeli timu yake kwa kuiita timu ya Harry Kane kitu ambacho Guardiola amekipinga na kusema Pochettino amemuelewa vibaya.

Pep amesema lengo lake la kuiita Tottenham kuwa ni timu ya Harry Kane ilikuwa ni kuheshimu mchango mkubwa unaotolewa na nyota huyo wa England kwenye klabu yake.

Baadae Pochettino alimjibu Pep akidai kuwa ameikosea nidhamu timu yake kwa kuiita timu ya Harry Kane na amekuwa na tabia ya kudharau timu za wenzake wakati yeye alipewa mafanikio na Messi akiwa Barcelona na hakuna aliyeita timu ya Messi.

Hata hivyo Pep amejibu tena leo asubuhi kwa kusema Pochettino ana chuki binafsi tangu wapo Hispania. Wawili hao wamekuwa wapinzani tangu wakiwa Hispania wakati Pep akiinoa Barcelona na Pochettino akiinoa Espanyol ambao ni wapinzani wa jadi katika jimbo la Catalunya.