Jumatatu , 14th Sep , 2020

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu nchini Tanzania TPLB ,Almasi Kasongo amewataka wamiliki wa viwanja vinavyochezewa Ligi Kuu soka nchini Tanzania VPL wajiandae na rungu kutoka bodi hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo akizungumza na Waandishi wa Habari.

Akiongea na Kipenga hii leo Mtendaji huyo amesema kuwa kwa viwanja vyovyote ambavyo vitakiuka sheria namba moja ya Sheria ya Mpira wa Miguu Ulimwenguni FIFA inayozungumzia uwanja kwaajili ya mchezo wa mpira wa miguu.

"Jambo zuri ambalo ninafurahia ni kuwa sisi sote kwa upamoja wetu tunaridhika kwamba hivi viwanja vilivyofungiwa kweli havikidhi viwango, havikidhi matakwa ya kikanuni ya sheria namba moja katika sheria namba 17 ya Mpira wa miguu." Amesema.

Itakumbukwa kuwa hadi sasa tayari viwanja viwili vimeshafungiwa kwa kutokidhi vigezo angu kuanza kwa msimu mpya wa VPL 2020-21 tarehe 06 Septemba mwaka huu, viwanja hivyo ni pamoja na uwanja wa timu ya Gwambinu uliopo Misungwi Mwanza na uwanja wa Musoma unaotumiwa na Biashara United

Aidha, CEO Kasongo amekiri kuwa upya wa mfumo wa kielektroniki katika kuingia viwanjani ndio chanzo ya changamoto iliyojitokeza siku ya jana uwanja wa taifa katika mechi ya VPL iliyowakutanisha Yanga na Mbeya City 1-0

"Kama unavyojua mzabuni ni mpya inawezekana 'experience' uzoefu huo hakuwa nao ila kadri mechi zinavyoendelea naamini wataenda kuwa bora lakini pia watazamaji wajitahidi kuingia mapema viwanjani." Amesema