Alhamisi , 21st Aug , 2014

Bodi ya ligi Tanzania TPLB imesema wanataraji kuwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara na ligi daraja la kwanza 2014/2015 utakuwa ni msimu wa mafanikio kuliko msimu uliopita wa 2013/2014

Baadhi ya viongozi wa juu wa TFF ambao watakutana na uongozi wa bodi ya ligi Tanzania TPLB.

Bodi ya ligi Tanzania TPLB imesema imepanga kufanyia marekebisho mapungufu yote yaliyojitokeza katika ligi kuu Tanzania bara VPL na ligi Daraja la kwanza FDL ili kuhakikisha ligi za msimu ujao zinakua bora zaidi ya msimu uliopita

Mjumbe wa Bodi ya ligi Dr. Damas Ndumbaro amesema pamoja na ligi ya msimu uliopita kuwa na mafanikio lakini ilikuwa na changamoto ambazo safari hii watakutana na shirikisho la soka nchini TFF ili kuzitatua

Ndumbaro amesema moja ya Changamoto ni uamuzi na mapungufu katika masuala ya usajili, ambapo kwa mamlaka ya bodi ya ligi hawakuwa na uwezo wa kumfungia mwamuzi anaye boronga zaidi ya kumfuta katika orodha ya kuchezesha ligi husika

Aidha Ndumbaro amesema katika vitu ambavyo havikuwa chini ya bodi hiyo ni suala la maamuzi ya kuwaadhibu waamuzi kwani suala hilo lilikuwa katika kamati nyingine ila wao walikuwa na uwezo wa kumfuta mwamuzi katika ratiba na si kumfungia lakini kwa upande wa makamishna walikuwa na uwezo wa kutoa adhabu yoyote kwa kuwa walikuwa wanawajibika moja kwa moja kwa bodi hiyo