Jumapili , 21st Mei , 2017

Tetesi za nahodha wa Azam FC na mshambulizi tegemeo John Bocco kuwa ametemwa na klabu yake ya Azam FC zinaendelea kuenea kwa kasi kila kona kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya maneno aliyoandika John Bocco kwenye mtandao wa kijamii

Kumekuwa na taarifa kwamba Azam FC wameamua kuachana na Bocco ambaye ameichezea klabu hiyo tokea ianzishwe.

Ambacho kinaonekana kuwashitua mashabiki ni Bocco kutupia maneno kadhaa ya mafumbo kwenye mitandao ya kijamii ambayo wengi wametafsiri kuwa huenda akawa anaaga.