Alhamisi , 27th Oct , 2016

Bondia Mtanzania Cosmas Cheka amesema, licha ya kupewa mpambano muda ukiwa umeenda lakini anaamini atapambana hapo kesho mpaka amuangushe mpinzani wake Jason Bedeman kutoka Afrika Kusini.

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Jay Msangi (Katikati) na Cosmas Cheka (kulia)

 

Cosmas Cheka ambaye anawania mkanda wa Bantam Weight uzito wa kilo 59 mpaka 61 wa raundi 10 amesema, amejipanga vizuri na yeye kama bondia muda wote ni wa mazoezi na anaamini atampiga mpinzani wake katika mpambano huo.

Kwa upande wake Meneja wa Cheka Juma Ndambile amesema, anaamini bondia wake atapambana kwa ajili ya ushindi kwani amemuandaa vizuri kwa ajili ya kuweza kuweka heshima ya ngumi katika ramani ya Tanzania.

Mbali ya mpambano huo lakini mpambano mwingine mkubwa hapo kesho utamkutanisha bondia Mtanzania Dullah Mbabe dhidi ya Chengbo Zheng kutoka Taifa la China ambao watapambana kuwania uzito wa Light-Heavyweight huku kukiwa na mapambano mengine matano ya utangulizi.