Jumatatu , 17th Jan , 2022

Nyota wa tenisi Novak Djokovic anaweza kurejea Australia mapema kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kuondoshwa kwake nchini humo kutokana na kukosa vigezo kwenye hati yake ya kusafiria, waziri mkuu wa nchi hiyo anasema.

Djokovic akirejea nchini Serbia baada ya kuzuiliwa kuingia Australia, kushiriki michuano ya wazi nchini humo.

Mchezaji huyo bora wa wanaume alirudishwa nchini kwao siku Jumapili baada ya hati yake ya kusafiria kukutwa na kasoro kutokana na kushindwa kuweka wazi kama amechoma chanjo ya UVIKO-19 au Lah!

Chini ya sheria za uhamiaji za Australia, Djokovic, 34, hawezi kupewa visa nyingine kwa miaka mitatu. Lakini Waziri Mkuu Scott Morrison alisema anaweza kuruhusiwa kuingia mapema chini ya njia stahiki.

" huchukua muda wa miaka mitatu, lakini kuna fursa ya wao kurejea vipenge vya vizuizi katika hali ifaayo na hilo litazingatiwa wakati huo utakapofika," alisema katika mahojiano na kituo cha redio cha Australia 2GB siku ya Jumatatu.

Hii inaweza kuruhusu Djokovic kushiriki katika mashindano ya Australian Open mwakani 2023, ambapo Djokovic anakosa michuano ya mwaka huu inayoanza leo kama bingwa mtetezi, na taji aliloshinda mara nyingi zaidi, mara nane