Ijumaa , 30th Dec , 2022

Kiungo wa zamani wa Klabu ya Young Africans na Azam FC Frank Domoayo ‘Chumvi’ ametambulishwa rasmi na Klabu ya Namungo FC ya mkoani Lindi.

Domayo amejiunga na Klabu hiyo akiwa mchezaji huru, baada ya kuachwa na Azam FC mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22.

Domayo ametambulishwa rasmi Klabuni hapo kupitia Kurasa na Mitandao ya Kijamii ya Namungo FC, huku taarifa hiyo ikiandikwa: #WelcomeTosouthernkillers

Karibu kwenye Familia ya Namungo Fc Frank Raymond Domayo

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa Namungo FC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, akitanguliwa na Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Stephen Sey.

Sey aliwahi kuitumikia Namungo FC msimu wa 2020/21 kabla ya kuondoka, baada ya kusajiliwa na Klabu ya Eastern Company SC ya nchini Misri.